Serikali ya Russia ilidai baada ya milipuko hiyo kuwa ni wapiganaji wa Chechnya waliohusika utegaji huo.
Milipuko hiyo iliua raia watatu na kujeruhi wengine 15 ambapo mlipuko wa kwanza ulitokea eneo la sokoni katika mji wa Vladi Kavkaz.
Taarifa za awali ziliotuhumu kuwa huenda bomu hilo lilikuwa limetegwa kwenye gari iliyoegeshwa katika soko hilo.
Mlipuko wa pili ulitokea katika mji wa Rostov alikozaliwa mhalifu wa kivita Budanov.
Taarifa kutoka kwa wapiganaji wa Chechnya zimetuhumu milipuko hiyo katika maeneo ya raia kuwa huenda ni mbinu ya kjasusi inayotumiwa na idara hiyo ya usalama ya Moscow kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi wa Russia dhidi ya Wachechnya na hasa kwa wapiganaji hao wa kiislamu.
Wachechen wamesema kuwa mbinu ya aina hiyo ndiyo iliyotumiwa na idara hiyo ya ujasusi ya Russia mwaka wa jana kuhalalisha kampeni yake ya kutaka kuifanya Chechnya koloni lake.
Taarifa hiyo ya wachechen imeeleza kuwa katika mashambulizi ya mwaka wa jana idara ya ujasusi ya Russia(FSB) iliripua majengo na nyumba kadhaa za raia mjini Moscow na miji mingine ya nchi hiyo.
Aidha imedai kuwa ushahidi kuwa idara ya usalama ya Russia ilihusika kuhujumu wananchi na miji yake uliripotiwa na Vyombo kadhaa vya habari duniani.
Muda mfupi baada ya kutokea mlipuko wa mwaka wa jana polisi ya Russia ilidai kuwakamata watu kadhaa ambao iliwatuhumu kuhusika na utegaji wa mabomu hayo katika majengo mjini Riyazan.
Hata hivyo baadhi ya waandishi wa habari wa mashirika ya nje na walinzi wa mgambo wa Russia walithibitisha kuwa watu hao waliokamatwa walitambulika baadaye kuwa walikuwa maajenti wa idara ya usalama ya Russia(FSB) na waliachiwa huru kwa amri serikali.
Akitoa agizo la kuachiwa watu hao, aliyekuwa waziri mkuu wa Russia, Stepashin alipongeza hatua hiyo ya kuwanasa watu hao lakini alidai kuwa walikuwa maajenti wa Intelligence ya nchi hiyo.
"Maajenti wa FSB waliokamatwa na baadaye kuachiwa walifanya zoezi hilo kwa sababu za kiusalama, alidai waziri huyo wakati akitoa agizo hilo.
Kwa upande wao wachechen kuhusiana na milipuko hiyo ya Vladi Kavkaz na Rostov jumapili iliyopita walitoa tamko lifuatalo kukanusha kuhusika na hujuma hiyo.
"Serikali ya Russia na Ulimwengu kwa ujumla unapaswa kujua kuwa Mujahidiin hawawezi kukana operesheni yoyote ya kijeshi waliyoifanya. Wanajivunia na kukiri bila ya woga wala unafiki operesheni zote wanazozifanya. Kama mujahidiin wangehusika katika milipuko hiyo ya Vladi Kavkaz na Rostov wanekiri wazi wazi; lakini kwa kuwa ulipuaji huo ni kinyume na maadili ya Uislamu ambayo yanakataza kuua raia wasio na hatia ni dhahiri kuwa mauaji hayo yamefanywa na wanajeshi makatili wa kirusi.
Hii ni vita kati yetu na majeshi ya uvamizi ya Russia; si vita baina yetu na wananchi wa Russia. Na tukitaka kufanya ulipuaji tunaelekeza kwa majeshi ya Russia nchini Chechnya na nje ya Chechnya".
'ESPIONAGE na counter intelligence' ni Istilahi mbili zilizokuwa maarufu miongoni mwa maafisa wa iliyokuwa KGB na majasusi wengine duniani zikiwakilisha utendaji uliolenga kujipenyeza kwa adui lakini ukitofautiana dhamira na mitazamo.
Espionage ilikuwa ni "ujasusi penyezi au pandikizi" dhidi ya makundi hatari kwa Dola hilo na Counter intelligence iliwakilisha "ujasusi dhidi ya ujasusi" uliofanywa na KGB dhidi ya mitandao mingine ya kiusalama au kijasusi ndani na nje ya Soviet wakati huo huo ikihakikisha yenyewe kutoingiliwa na mitandao ya adui.
Kwa mujibu wa vitabu "spy counter spy" kilichonukuliwa na "the faber book of espionage" na "The practice of Recruiting Americans in the USA and Third Countries", Counter intelligence ilikuwa istilahi iliyowakilisha vita ya kitaaluma baina ya KGB na mashirika mengine hasa CIA ambayo ilichukua hata miaka 10 kwa ajenti kufikia lengo ndani ya mtandao wa adui hasa kushika nafasi za kimaamuzi. KGB ilikuwa maarufu kwa ujasusi wa malengo ya muda mrefu.
Kitabu "The practice of Recruiting Americans in the USA and Third Countries" kimeandika ujasusi penyezi na pandikizi (espionage) , ulikuwa mtandao muhimu uliotumiwa na KGB('KGB espionage network') kupata habari juu ya harakati na minong'ono na mipango ya makundi, jumuiya au taasisi, mashirika ya serikali, yasiyo ya serikali, vilabu vya michezo, vya burudani, dini nakadhalika
Ujasusi huu ulilenga vyote kupata habari au kudhibiti harakati zote hatari(surbversive) dhidi ya 'system ya Soviet' ambao uliwezekana kwa maafisa wa KGB kujipenyeza au kuwa na maajenti katika taasisi au makundi hayo wakiwapa habari zote kabla ya hatua za muhimu kuchukuliwa.
Waliohusika na operesheni hiyo ama walikuwa maafisa wenyewe wa KGB waliojipenyeza moja kwa moja(Direct penetration) kwa mbinu mbali mbali kuwa kama watendaji, wanachama, viongozi wa juu ndani ya makundi, au kutumia maajenti(infiltration) walio kuwa na maajenti walio miongoni mwa wafuasi, wanachama au wahusika wa taasisi, makundi, mkusanyiko, taasisi, jumuiya au shirika husika.
Kikielezea madhumuni ya ujasusi penyezi, kitabu the secret work of Soviet secret Agents kimeandika ujasusi pandikizi na penyezi (Espionage) huweza kutumika ili kuzuia mashambulizi ua uvamizi wa ghafla kutoka kwa adui hali kadhalika husaidia kumshambulia adui kabla hajatekeleza mpango wake.
Kwa madhumuni hayo KGB na mashirika mengine makubwa ya ujasusi yamekuwa yakitumia Espionage kuchunguzana yenyewe kimataifa au kudhibiti nyendo zilizoonekana kuhatarisha maslahi ya nchi na watawala wake au kutaka kujinufaisha kisayansi na teknolojia, kisiasa na kijeshi.
"Kwa miongo kadhaa KGB iliajiri kimya kimya majasusi iliowapa mafunzo ya kina ya Espionage iliyowatumia kuiba ufundi wa kisayansi, kiviwanda na kijeshi kutoka nchi za kigeni. Vile vile iliwatumia majasusi hao kupata maajenti katika nchi hizo walioweza kuchochea migogoro na hatimaye machafuko kwa maslahi ya Soviet", ameandika mwandishi maarufu wa masuala ya ujasusi bwana Barron.
Espionage ilikuwa moja ya shughuli zilizowachukua muda mrefu maafisa wa KGB nje ya nchi yao. Mnamo mwaka 1945 ikitumia taaluma hiyo Soviet ilidaiwa kuiba teknolojia ya utengenezaji wa bomu la Atomic nchini Marekani.
Sambamba na wizi huo, tume maalum zilizoundwa katika nchi za Canada na Austria na uchunguzi wa kiserikali uliofanywa katika nchi za Uingereza na Marekani ulibainisha kwamba Soviet ilikuwa na makachero ndani ya serikali za nchi za magharibi, katika taasisi za kisayansi na duru za kisomi za nchi hizo.
Kitabu maarufu kiitwacho KGB kilichoandikwa miaka 26 iliyopita (1974) kimewataja baadhi ya maajenti wa Soviet waliokamatwa nchini Marekani wakifanya Espionage katika idara na taasisi mbali mbali za nchi hiyo.
Maajenti waliotambulika walikuwa ni pamoja na Elizabeth T. Benteley, Edward Joseph Fitzgerald, William Ludwig Ullmann, William Walter Remington, Franklin Victor Reno na Judith Coplon.
Wengine waliotajwa na kitabu hicho cha mwaka 1974 walikuwa ni Hary Gold, David Greennglass, Julius, Ethel Rosenberg, Morton Sobell, William Perl, Alfred Dean Slack, Jack Soble, Ilya Wolston, Alfred na Martha Stern.
Pamoja nao alikuwemo aliyekuwa mhariri wa jarida la Time ambaye ilidaiwa alikiri kuwa alikuwa ajenti wa KGB na kumtaja mshirika mwenziwe Alger Hiss.
Wote hao walikuwa Waamerika lakini wakiwa katika Payroll ya KGB
Maajenti wa KGB waliogundulika nchini Uingereza walikuwa ni pamoja na mtaalamu wa fizikia ya Nyuklia Klaus Fuchs na mwenzi wake Allan Nunn May. Walikuwemo pia wanadiplomasia mabwana Gy Burgess na Donald Maclean. Kadhalika alikuwemo Harold A. R. Philby aliyekuwa afisa mwaandamizi wa idara ya ujasusi ya Uingereza(M16).
Ujerumani pia iliwahi kudai kuwa mmoja wa wanasayansi wake wa kuaminika, Joseph Eutzernberg alikuwa ajenti wa KGB kwa muongo mzima.
Ufaransa ilimnasa mhandisi wa nguvu za atomic, Dmitri Volokov ikimshuku kuwa alikuwa ajenti wa KGB kwa miaka kadhaa. Volokov alishukiwa kuiba na kutorosha nyaraka kadhaa za kiufundi zilizohusiana na utafiti wa kinyuklia wa Ufaransa.
Aidha Norway ilimfukuza Afisa wa kirusi Valeri Nikolaevich Yeroveyev ambaye akiwa nchini humo alijitambulisha kama mwanadiplomasia. Ilimnasa akiwasajili raia wa Norway kuwa majasusi (maajenti wa KGB waliokuwa wakiripoti kwake).
Kikifafanua utekeleza wa Espionage nje ya Soviet kitabu cha kiada cha KGB kiliandika ifuatavyo.
"Our intelligence officer must establish confidential relations with the..... in such a way that the latter does not surmise his connection with Soviet Intelligence and his true intentions".
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |