MWENYEZI Mungu aliyetukuka, kwa kuwa yeye ndiye aliyewaumba wanadamu na kuwaneemesha neema zisizo na hesabu, ana haki ya kuwahalalishia na kuwaharimishia anachotaka, kama vile vile alivyokuwa na haki ya kuwalazimisha wamuabudu kwa njia anayotaka,wala wao hawana haki ya kupinga au kuasi, kwani hii ni haki ya Uola wake juu yao na kustahiki kwake kuabudiwa na wao.
Pamoja na hayo, Mwenyezi Mungu aliyetukuka kwa sababu ya rehema zake juu ya waja wake, amejaaliya kuhalalisha na kuharamisha kwa ila na sababu fulani ambazo ni kwa mslaha ya wanadamu wenyewe, akawa hakuhalalisha jambo ila kwa kuwa zuri na hakuharimisha jambo ila ni kwa kuwa ovu.
Ni kweli kuwa Mola aliuharimishia umma wa Kiyahudi baadhi ya vitu vizuri, lakini huko kulikuwa kwa sababu ya kuwatia adabu kwa uovu wao na kuvunja kwao matakaso ya Mwenyezi Mungu kama alivyosema:
Na kwa wale walio Mayahudi tuliharamishia kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tukawaharimishia shahamu (mafuta) yao isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao au ile iliyogandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao, na bila shaka sisi ndio wakweli (sio wao wanaojidai kuwa Mungu hakuharamisha haya kwa ajili ya ubaya wao; lakini wenyewe tu wazee wa Kiyahudi waljiharamishia haya, na wao chipukizi zao wakafuata). (Al-An-am: 146).
Vile vile, amebainika uovu wao huu katika sura nyingine, akasema:
Basi kwa dhulma yao hao Mayahudi tuliwaharimishia vizuri walivyohalalishiwa na (vile vile) kwa sababu ya kuzuilia kwao watu wengi na njia ya Mwenyezi Mungu. Na kwa sababu ya kula kwao riba ilhali wamekatazwa wasiile, na (kadhalika) kwa kula kwao mali za watu kwa batili. (An-Nisaa: 160-161).
Hata Mwenyezi Mungu alipomleta Mtume wake wa mwisho na dini yake ya milele kwa watu wote, ilikuwa ni kwa rehema yake Mola juu ya wanadamu, baada ya kupevuka na kuwa tayari, kuwaondoshea uzito wa kuharimishiwa uliokuwa kwa sababu ya kutiwa adabu watu walioasi kwa muda fulani, kama ilivotajwa katika Taurati, na ukawa ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.) kwa watu wa Kitabu ni kama ulivyoelezwa katika Qur'an:
Ambaye wanamuona ameandikwa kwao katika Taurati na Injili ambaye anawaamrisha mema na anawakataza mabaya na kuwahalalishia vizuri na kuwaharimisha vibaya, na kuwaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao ( yaani Sharia ngumu za zamani na mila za kikafiri). (Al-Aaaraf: 157).
Mwenyezi Mungu kisha akaweka sharia ya kutubia makosa katika Uislamu kwa kufanya mambo mengine badala ya kuharimisha mazuri. Kwa mfano kuna toba ya dhati ambayo inafuta madhambi kama yanavyoondoa uchafu maji, na kuna mema ambayo huondoa na kuyafuta maovu, na kuna kutoa sadaka ambako kunayazima makosa kama unavyouzima moto maji, kuna na matatizo na masahibu ambayo yakimfika mtu hupeperusha makosa yake kama yanavyopeperushwa majani makavu ya miti katika majira ya baridi.
Kwa hivyo, imekuwa inajulikana katika Uislamu kuwa kuharimishwa jambo ni kwa sababu ya uovu wake na madhara yake, basi lile ambalo lina madhara matupu huwa ndilo la haramu, na lile ambalo madhara yake ni makubwa kuliko manufaa yake huwa ni haramu, na lile ambalo linalomanufaa zaidi kuliko madhara huwa ni halali, na haya ni yale ambayo Qur'an tukufu imeyaeleza kuhusu ulevi na kamari.
Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: "Katika hivyo mna madhara makuu na (baadhi ya) manufaa kwa (baadhi ya) watu. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manu Mungu, kwani huenda usijulikane uovu wa kitu fulani katika zama zake, ukaja ukadhihiri katika zama nyingine zijazo na juu ya mwenye kuamini kusema daima: "Tumesikia na tumetiii".
Je, huoni ya kuwa Mwenyezi Mungu ameharamisha nyama ya nguruwe na Muislamu asijue ubaya wa kuharamishwa isipokuwa ya kuwa ni mchafu, kisha siku zikapita, ilimu ikaja kugundua kuwa ina vidudu na viini vya hatari. Bali hata ilimu ingekuwa haikufichua hakika hii au amegundua zaidi kuliko haya, Muislamu atabakia na itikadi yake ile ile ya kuwa nguruwe ni najisi na haramu.
Na mfano wa haya, Hadithi ya Mtume (s.a.w) isemayo (Ogopeni laana tatu) yaani yale mambo ambayo mwenye kuyafanya humletea laana ya Mwenyezi Mungu na ya watu. Kukidhi haja katika (sehemu tatu) katika vidimbwi vya maji, katikati ya njia na katika kivuli cha mti au kitu chochote kile). Amesimulia Abu Daud na Ibn Majah na Al-Hakim na Bayhaki.
Wala hapana aliyekuwa akijua katika zama zilizopata madhara yake ila kuwa ni katika mambo machafu anayojitenga nayo mtu mwenye murua wake na adabu zake. Hata ulipoendelea uchunguzi wa kisayansi tumejua kuwa haya mambo matatu yalolaaniwa ni katika mambo ya hatari sana juu ya siha na afya ya jamii, nayo ni chanzo cha kwanza cha kueneza maradhi ya kuambukiza kama kichocho, na kadhalika.
Na hivi ndivyo ilivyo. Kila ikizidi ilimu na kuvumbuliwa mambo mapya, tunazidi kufahamu faida ya Uislamu katika mambo ya halali na haramu, na mambo mengine yanayohusu sharia ya Mwenyezi Mungu. Na kwanini isiwe hivyo nayo ni sharia ya Mjuzi Mwenye Hekima na Mrehemevu juu ya waja wake.
Na Mwenyezi Mungu anamjua fisadi na mtenda
mema, na angelipenda Mwenyezi Mungu angelikutieni katika udhia. Hakika
Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu na mwenye hekima. (Al-Baqara: 220).
--
![]()
|
|