SAMI Sharaf alikuwa mshauri wa kiusalama wa aliyekuwa Rais wa Misri Dikteta Jamal Abdul Nasser.
"Alikuwa ni mwenye nafasi yake katika serikali ya Nasser. Mtu aliyekuwa akisikilizwa na kuaminiwa zaidi na Rais huyo. Yeye ndiye aliyekuwa muandaaji wa mikakati yote ya kijasusi na kiusalama nchini humo", anaeleza afisa mmoja wa iliyokuwa idara ya usalama ya Misri zama za utawala wa Nasser.
Sharraf alikuwa mmoja wa maajenti muhimu wa KGB ulimwenguni. Akiwa mwenye urefu wa futi tano na nchi sita, umbile la kawaida na sharubu zilizoangukia mdomo, KGB ilimtegemea kwa akili yake shapu na kipaji cha ubunifu.
Akichelea kuhusishwa na uhalifu hasa uhaini, hakuwa na marafiki wa kudumu. Maeneo aliyokuwa akipendelea kufika nyakati za jioni akiwa na mkewe ilikuwa katika majumba ya sinema.
KGB ilianzisha uhusiano wa karibu na Sharraf mwaka 1955 alipotembelea Moscow kwa ziara iliyokuwa imelenga kuanzisha uhusiano wa kijeshi kati ya Misri na Soviet.
Baada ya ziara hiyo, aliyekuwa mkuu wa baraza la mawaziri la Misri, mkomunist Ali Sabry alimteua Sharaf kuwa msaidizi wake. Inadhaniwa alifanya hivyo kufuatia ushauri wa siri wa Soviet.
Akiwa msaidizi wa Mkuu wa baraza muhimu nchini humo, Sharaf alitumia nafasi hiyo kuwa karibu zaidi na Rais Nasser.
Aliitembelea tena Soviet mwaka 1957 akiongoza wajumbe wengine wa nchi hiyo, KGB ilipata fursa ya kumuangalia na kumpima zaidi. Baada ya ziara hizo mbili za Soviet, Sharraf alizuru NewYork mwaka 1958 ambako mara mbili alipata fursa ya kukutana kwa siri na Vladmir Suslev, afisa wa KGB aliyekuwa mjumbe wa Soviet Umoja wa Mataifa.
Pamoja na kumfahamu vyemaKGB haikumwita kwa jina lake halisi ajenti wake huyo muhimu, katika makao makuu ya shirika hilo la kijasusi mjini Moscow alijulikana kwa 'code name' Asad. "Alitambulika kama simba(Asad)".
Akijificha kwenye "shadow" wadhifa wa ukurugenzi wa ofisi ya habari iliyokuwa chini ya Rais Nasser, Sharaf ndiye hasa aliyeongoza idara ya usalama ya Misri kuanzia mwaka 1959, na pia ndiye mshauri mkuu wa usalama wa Rais Nasser.
Kuanzia wakati huo akajiweka mbali na Sabry akiendesha shughuli maalum ya KGB nchini humo. Akishirikiana na Rais Nasser, Sharraf alitoa tenda ya mafunzo ya maafisa wa usalama wa Misri kwa Soviet.
Mpango huo wa mafunzo ya kwa maafisa wa "intelligence" ya Misri ilikuwa fursa nzuri kwa KGB kupenya ndani ya serikali ya nchi hiyo.
"Mpango huu wa mafunzo ulimpa fursa pia Sharraf kukutana wazi wazi na aliyekuwa afisa wake wa KGB mjini Cairo, Vadim Kirpichenko", anaeleza mtaalamu mmoja wa ujasusi katika mada yake Secret from the Desert.
Mnamo miaka ya 60, Sharraf ndiye aliyekuwa akiidhinisha shughuli za utumishi nje ya nchi hiyo, ndiye aliyekuwa akikagua na kusimamia shughuli zote za usalama na upelelezi kwa wafanyakazi wa serikali na ndiye aliyekuwa akiendesha operesheni zote za nje za idara ya usalama zilizokuwa na maslahi binafsi ya Rais Nasser huku akiwa ajenti mahiri na mwaminifu kwa KGB.
"Kwa madhumuni hayo aliunda mtandao (kitengo) maalum wa maafisa wa idara ya usalama wa nchi hiyo waliokuwa wakiripoti moja kwa moja kwake", imeelezwa katika makala hiyo ya kijasusi.
Kwa hiyo kupitia Sharraf KGB ndiyo iliyokuwa ikiiendesha idara ya usalama ya Misri miaka ya 60 ambayo Rais Nasser aliitegemea sana kimaamuzi na katika kupanga sera za kitaifa za nchi hiyo.
Ni katika miaka hiyo ndipo ilipoendeshwa operesheni dhidi ya wanaharakati wa kiislamu wa Ikhwan Muslimiin, maelfu ya vijana wa kiislamu waliotuhumiwa kuwa ni wanachama wa kundi hilo walikamatwa na kuwekwa magerezani, wengine kadhaa waliikimbia nchi hiyo kufuatia msako huo wa kinyama wa Rais Nasser na idara yake ya usalama chini ya maelekezo na ushauri wa KGB kupitia ajenti wake huyo mkuu bwana Sharraf.
Katika saka saka hiyo waliokamatwa ni pamoja na waliokuwa viongozi wa jumuiya hiyo Ismail al Hudhaibi, Shahiid Abdul Qaadir Awda, Abdul Fattah Ismail, Muhammad Yusuf Hawash, Bibi Zaynab al Ghazali na aliyekuwa mwandishi mahiri wa vitabu vya kiislamu na mfasiri bingwa wa Qur'an Shahiid Sayyid Qutb Ibrahim.
Baadhi ya wanaharakati hao walihukumiwa vifungo vya maisha na wengine akina Ismail Hudhaibi, Abdul Qaadir Awdah na Sayyid Qutb(radhiallahu Anhum) waliuawa wakidaiwa kuhatarisha usalama wa Taifa na kuandaa njama za kupindua serikali na kutaka kumuua Jamal Abdul Nasser(laanatullahi alahi ilaa yaumiddin).
Baadhi ya waandishi wa masuala ya usalama duniani wanamtaja bwana Sharraf kuwa baada ya kuvunja uhusiano wa Misri na nchi za magharibi, kwa maelekezo ya KGB ndiye alichochea maandamano ya Mwezi Novemba 1967 nchini humo ambayo kilele chake ilikuwa kuchomwa moto maktaba ya Marekani iliyokuwepo mjini Cairo.
|
|