Nchi yaingia doa
Ukweli marufuku Tanzania
Baada ya kufanya utafiti wa kisayansi mwandishi wa kitabu hicho ambaye ni mwanataaluma na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ametoa ushahidi huo bila chuki wala jazba. Vipi leo Rais Mkapa awe wa mwanzo kuwazuia wananchi kuusoma na kuupima ushahidi huo?
Katika kitabu hicho mwandishi amesema (na kutoa mifano) kuwa yapo madhila mengi ambayo Waislamu hutendewa hapa nchini ambayo Wakristo walio wengi hawajui ku a mambo mengine kilifichua njama na dhulma wanazofanyiwa Waislamu nchini. Mpaka hivi hakuna mwanachuoni aliyeuhoji ushahidi huo. Kitabu hicho hakikupigwa marufuku.
Ni hivi juzi tu kwa mara nyingine tena Kanisa Katoliki limechapisha na kusambaza nchini kitabu Uchaguzi Mkuu: Kwanini Tujali? Kitabu hicho kinatoa shutuma nzito dhidi ya CCM na serikali yake. Hakikuifurahisha CCM wala serikali, lakini kwa kuwa kimeandikwa na wanataaluma Wakatoliki, hakikupigwa marufuku.
Na huko nyuma tangia mwaka 1981 Kanisa limekuwa likisambaza kitabu kilichodhaminiwa na Kanisa na kuandikwa na Jan Pvan Bergen kiitwacho Development and Religion in Tanzania. Katika kitabu hicho kumechapishwa mazungumzo ya siri yaliyofanywa baina ya Hayati Mwalimu Nyerere na Askofu Robert Rweyemamu wa Kanisa Katoliki yaliyohudhuriwa pia na aliyekuwa mwakilishi wa Papa nchini, Givano Cerano.
Kwa mujibu wa kitabu hicho Nyerere alichukua ahadi ya kutumia madaraka yake ya kisiasa kuimarisha Ukatoliki nchini. Kitabu hicho hakijapigwa marufuku. Kiliandikwa na kusambazwa na Wakristo, labda pengine wao ni raia wa daraja la kwanza.
Katika kitabu kilichopigwa marufuku, Dk. Hamza Njozi anasema japo kinadharia katiba inalinda haki na uhuru wa raia wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote, katika hali halisi ya utelekezaji mara nyingi dini ya mtu hutumika katika kuamua kama apewe au anyimwe haki yake ya kikatiba.
Uamuzi wa serikali wa kukipiga marufuku kitabu kilichoandikwa na mwanataaluma Muislamu unasadikisha maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Na ndio maana serikali imeshindwa japo kutamka sababu ya kukipiga marufuku kitabu hicho.
Na ili kuhakikisha kuwa hakuna shirika lolote lisilokuwa la kiserikali katika hayo mashirika yanayotetea katiba na haki za binadamu litakalosimama japo kulaumu hatua hiyo ya serikali, baadhi ya vyombo vya habari vimeanza kukiita kitabu hicho kuwa "NI KITABU CHA WAISLAMU". Ujumbe unaotolewa na vyombo hivyo vya habari ni kuwa, kwa kuwa kitabu hicho ni cha Waislamu hakuna haja ya kuilaumu serikali hata kama ni kinyume na katiba. Tangu lini Muislamu akawa na haki kama raia wengine?
Tunaamini utamaduni huu wa kuwabagua raia kwa misingi ya dini zao utaitumbukiza nchi yetu katika janga la kisiasa.
Iwe itakavyokuwa tunadhani hatua hii ya Rais imeutia doa kubwa uongozi wake na nchi yetu. Na wanaodhani kuwa hakuna haja ya kuikemea serikali kwa kuwanyima raia haki yao ya kupata habari kwa sababu kitabu chenyewe ni cha Waislamu, wanajidanganya.
Ukweli kadri utakavyofichwa utaibuka tu. Siasa za ghilba hazijengi. Siasa za wale watamanio kudumisha maslahi binafsi na 'watu wao' ya muda mfupi bila kuzingatia maslahi ya kudumu ya Taifa.
Tunaamini raia wema wataendelea kuifichua dhulma na uonevu, na kufanya juhudi kusimamisha haki na uadilifu ili kuinusuru nchi yetu na matokeo mabaya ya ubaguzi na ukandamizaji.
Matokeo yanayoendelea kutoza ushuru wa roho
za watu huko Rwanda, Burundi na Kossovo.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |