Usikilizaji mzuri


Utafiti umeonesha usikilizaji wenye tija hutegemea mambo muhimu

yafuatayo:

Ubunifu katika akili ya msikilizaji

Uoni wa haraka

Akili huria, iliyoepukana na uhafidhina (ubishi, ukaidi, msimamo na mazoea)

Kuepuka kutathmini hotuba au maelezo kabla ya kusikiliza habari inayowasilishwa hadi mwisho.

Si kila msikilizaji hunufaika na kile alichokisikia. Nukta zifuatazo zaweza kusaidia kuinua kiwango cha usikilizaji wetu:

a) Kwa kawaida kila habari, hotuba au mawaidha lipo jambo linaloweza kuvuta akili ya msikilizaji bali kuna watu wasio na mvuto. Kwa hiyo ni muhimu kutafuta nukta ya kuvutia kisha ukaizingatia.

(b) Usikilizaji mzuri ni ule unaojiepusha na chuki zisizo na msingi (prejudice). Hata kama anayehadhiri au kueleza ni yule msiyeafikiana, au kimaumbile si mzungumzaji mzuri jaribu kuuweka sawa ujumbe huo. Zingatia "alichokizungumza siyo namna alivyozungumza". Mara zote chuki isiyo na msingi huviza akili.

(c) Kuwa na lengo katika usikilizaji. Kutokutathmini ujumbe mpaka ufike mwisho. Kutokuwa na jazba dhidi au juu ya neno lolote linalopinza au kuchochea hisia.

Msikilizaji mzuri ni yule anaezingatia kiini cha fikra iliyowasilishwa na hubaini mwenendo wa lugha ilinayotumiwa na muwasilishaji. Huwa mwepesi kutenga ukweli na mambo ya msingi, mifano, ushahidi na hoja.

Msikilizaji huyo hubadilika baada ya kuzingatia kweli, mambo ya msingi, fikra, mifano, ushahidi na hoja anazopewa, kadhalika huwa makini kubaini kauli zisizowazi au zenye kutatanisha.

Usikivu na umakini wake humfanya mzungumzaji awe makini na mwangalifu katika uzungumzaji wake, vile vile umakini huo waweza kumchochea kutoa zaidi anachokijua katika jambo analoliwasilisha.

Kujizuia na jambo lenye kuhamisha mazingatio. Fikra zisivutwe mahala pengine au nje ya kile kilichokusudiwa kusikilizwa wakati ule.

Kusaidia kukuza kasi ya uoni jaribu kufanya yafuatayo

- Jaribu (kiakili) kumtangulia mzungumzaji kwa kuzingatia kauli aliyoizungumza mwanzo, kuelewa nini atazungumza mbele au hitimisho la mazungumzo yake.

- Fupisha kile alichozungumza.

- Pima uzito wa ushahidi uliotolewa kuthibitisha nukta fulani.

Fikiria maana iliyofichikana au kuwa na tafsiri nyingi juu ya jambo lililowasilishwa.

Fichua maana ya ndani ya kila neno au maneno yaliyotumiwa.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org


An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook