GAZETI la UHURU la Ijumaa Julai 28, 2000 liliripoti kuwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kushirikiana na Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) limeandaa wahamasishaji 17,550 watakaosambaa nchi nzima kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura ili wajue haki na wajibu wao katika kushiriki katika uchaguzi huo.
Mratibu wa zoezi hilo, Peter Maduki alisema katika ukumbi wa CCM, washiriki 22 watatoa mafunzo katika mikoa ya Singida, Tabora na Dodoma.
CCT na TEC iliandaa semina 210 kanda ya Ziwa mashariki, nyaza za juu, kusini mashariki na magharibi. Alisema, Kanisa limeamua kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha wananchi kuchagua viongozi bora.
Tunaona jinsi kanisa linavyoshiriki kikamilifu katika siasa ya nchi hasa kwenye uchaguzi mkuu, lakini hatusikii kauli za kuonywa kuwa wasichanganye dini na siasa kama wanavyoshutumiwa Waislamu.
Wametamka wazi kuwa lengo lao ni kupatikana viongozi bora, hapana shaka yoyote kuwa viongozi hao ubora watapatikana katika Biblia kama alivyosema kiongozi mmoja wa Kanisa kule Tabora kuwa viongozi wazuri someni Biblia "Matendo ya Mitume".
Tukiangalia Tume ya Uchaguzi Wakristo wote, Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wote wamejaa watu wa dini moja (Wakristo), vile vile wahamasishaji tunapata mashaka makubwa kutendeka haki na usawa.
Gharama hii ya kanisa si ya bure kuna lengo lake. Hakuna anayefanya jambo lolote bila ya lengo maalumu. Wanaposema hali ya nchi nzuri kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni yote huwa ni kujitetea wao kama jamii ya Kikristo. Kila aliyae hushika kichwa chake.
Jumuiya na taasisi za Kiislamu mbona mko kimya kuhusu uchaguzi? Changamoto iko mbele yenu wahamasisheni Waislamu washiriki katika uchaguzi ili kupata viongozi wacha Mungu.
Haya shime BAKWATA, BARAZA KUU, Shura ya Maimamu, Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu, MSAUD, TAMPRO, AL-MALLID, na Tabligh kazi kwenu.
Malalamiko ya Waislamu yamekuwa mengi sana juu ya kutotendewa haki, sasa wakati ndio huu wa kuchagua viongozi watakaotenda haki kwa raia wote bila ya ubaguzi wa kidini, kabila au sehemu anayotoka mtu.
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |