TLP yadaiwa ni chama cha kikatoliki


MWENYEKI Bwana Makaidi alitoa dai hilo mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa MAELEZO jumatatu wiki hii.

Amesema kwa kuwa TLP ina uelekeo wa kidini chama chake hakiko tayari kuwa na ushirikiano nayo.

Alisisitiza kuwa chama chake kinaogopa udini, ukabila na ubinafsi kwa hiyo hakiko tayari kuungana na Bwana Mrema.

Alidai bendera ya TLP ina rangi ya manjano na nyeupe ambazo zinapatikana katika bendera ya Vatican ambako ni makao makuu ya Kanisa Katoliki Duniani.

Naye Bwana Abubakar Olotu Mwenyekiti wa chama NRA alikataa muungano na TLP kwa sababu hizo hizo.

Kauli za viongozi hao zimekuja wakati ambapoMwenyekiti wa TLP bwana Agustino Mrema amekuwa akitoa madai kuvishutumu baadhi ya vyama kuwa vina udini hali iliyomfanya asite kuungana navyo.

Hata hivyo Bwana Mrema hajaweza kuyitolea ushahidi madai yake hali iliyopelekea wafuasi wake wengi kukihama chama huku wakishutumu kile walichokiita ubinafsi na ukabila uliochanganyika na udini uliojikita katika nafsi ya Mwenyekiti wao.


Prince Charles atembelea shule ya Kiislamu London

LONDON, Uingereza

"Ninyi ni mabalozi wa imani ambayo kwa kipindi fulani haikuwa ikieleweka vyema"

Prince Charles ameyasema hayo hivi karibuni alipotembelea shule ya msingi ya Islamia iliyopo Jijini London nchini Uingereza.

Shule hiyo inayoendeshwa kwa ruzuku kutoka serikalini inasimamiwa na aliyekuwa muimbaji maarufu wa miziki ya Pop miaka ya sabini Cat Steven ambaye hivi sasa amesilimu.

Prince huyo wa Wales amempongeza Cat ambaye hivi sasa anajulikana kwa jina la Yusuf Islam, kwa uamuzi huo wa kusilimu na ambao alioufanya mwaka 1977.

"Naamini Uislamu una mengi ya kuzifundisha jamii za kisekula kama hii yetu ya Uingereza", Prince Charles alimwambia Yusuf Islam.

Mtoto huyo wa Malkia wa nchi hiyo alimdokeza Yusuf Islam kuwa yeye ni miongoni mwa waliokuwaa wapenzi wa miziki ya Pop zama za Cat Steven.

"Aliniambia alikuwa mpenzi wa Cat Steven, ameeleza Yusuf Islam baada ya ziara hiyo ya Charles katika shule hiyo ya msingi ya Waislamu.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook