Edward Spiro:
Jasusi gwiji la Kiyahudi

Kabla ya vita kuu ya kwanza Edward Spiro alikuwa mmoja wa maajenti wakubwa wa shirika la ujasusi la SIS (British Secret Intelligence Service (M16).

Wakati huo akiishi kwa kufanya kazi ya uandishi wa habari wa kujitegemea akiandikia magazeti mbali mbali ya nchi hiyo akiwa mwenye asili ya kiyahudi aliye na uraia wa Austria.

Mahusiano ya Spiro na SIS yalianza nchini Austria baada ya kuhitimu katika chuo kikuu cha Vienna wakati huo akiwa mhariri wa masuala ya siasa wa gazeti moja la jioni la nchi hiyo.

Mnamo mwaka 1936 alifanywa kuwa "Source" wa SIS na aliyekuwa mkuu wa kitengo cha shirika hilo nchini Austria Captain Thomas Kendrick.

Ilikuwa ni fursa hii ya ushushu iliyomuwezesha kuikimbia nchi hiyo na kuwa mkimbizi nchini Uingereza.

Kama wayahudi wengine waliokimbilia nchini humo, Spiro hakuwa na japo senti moja katika mfuko wake kwa hiyo alihitajika kufanya kazi ya ziada katika awamu hii ya maisha ya ukimbizini.

Kabla ya kujificha katika "mwavuli" wa uripota wa gazeti la Daily Telegraph katika bunge la nchi hiyo, Jasusi huyo wa kiyahudi alijipenyeza kwenye makundi ya Manazi kuwajibika katika shughuli yake ya siri ya uajenti wa SIS.

Jukumu lake katika makundi hayo kama ajenti lilikuwa kupeleleza wanachama waliomstari wa mbele na majasusi waandamizi wa kinazi waliomo kwenye makundi hayo.

Akiwa mmoja wa "wanachama waliomstari wa mbele" akifahamika kwa jina la E.H.Cookridge, Spiro aliajiriwa kwa kazi ya propaganda katika wizara ya ustawi wa uchumi ambayo ilikuwa idara ya serikali ya nchi hiyo iliyokuwa ikirusha propaganda dhidi ya Ujerumani.

Baada ya vita kuu ya pili kwisha mwaka 1945, Spiro aliandika kwa mapana fani ya Espionage akielezea maisha ya ushushushu ya Kim Philby na George Blake.

Spiro anaelezkatika kitabu hicho kuwa alimfahamu kwa mara ya kwanza Kim Philby mjini Vienna mwaka 1933 wakati huo wote wakiwa wafuasi wa harakati za chini chini zilizokuwa zikipinga udikteta.

Katika kitabu hicho, Spiro ambaye alifariki mwaka 1979 anaelezea urafiki wake na Kim Philby.

"Niliishi Vienna maisha yangu ya utoto na ujana ambako baba yangu alikuwa mwakilishi wa Kampuni ya nguo ya Manchester textile firm of Riddaway & Co.

Akiwa Chuo kikuu cha Vienna, Spiro anasema alikuwa akichukua kozi ya rerum politicarum, wakati huo huo akiwa ripota katika gazeti moja toleo la jioni, baadaye akahamishiwa toleo la asubuhi.

"Kitaaluma magazeti ya asubuhi huhitaji umakini zaidi kwa sababu bongo za wasomaji huwa tulivu kulinganisha na magazeti ya mchana, kwa hiyo sisi waandishi wachanga tuliwekwa kwenye magazeti ya mchana", anasema mwandishi jasusi Edward Spiro.

Spiro anasema magazeti hayo hayakuwa yakimilikiwa na chama cha "Social Democratic" lakini yalikuwa yakiziunga mkono sera za chama hicho kama magazeti ya Daily Herald na Daily Mirror yalivyokuwa yakikiunga mkono chama cha Labour.

"Nikawa ripota wa masuala ya Bunge na baadaye nikiwa na umri wa miaka 25 nikawa mhariri wa masuala ya siasa wa gazeti hilo", anaeleza jasusi huyu aliyefiachama katika kivuli cha uanahabari.

Akiwa mwanafunzi, anaeleza Spiro alikuwa mwanachama wa Klabu ya Social Democrat iliyokuwa chuoni hapo kisha akawa mmoja wa viongozi wa Klabu hiyo iliyokuwa na mrengo wa mageuzi na baadaye alikuwa mwanachama wa kawaida.

"Mnamo mwezi Februari, gazeti letu lilifungiwa na wahariri wote wakawekwa rumande. Mimi nilikuwa mmoja wa waliowekwa mahabusu, pamoja nasi walikuwemo baadhi ya wanasiasa", Spiro anasema.

"Nikilinganisha na uzoefu wangu wa ufungwa katika magereza ya Dachau na Buchenwald miaka kadhaa iliyopita, mahabusu ya Wollersdorf niliiona kama ni mahali pa mapumziko", anaeleza Spiro katika kitabu "upelelezi pandikizi".

Spiro aliachiwa wiki chache baadaye baada ya kukosekana ushahidi wa katika kesi ya kutaka "kufanya mapinduzi".

Hata hivyo alijikuta hana kazi baada magazeti yote ya wajamaa na maliberali kufungiwa yakidaiwa kuandika uchochezi dhidi ya serikali.

"Nilifanikiwa kupata ajira katika kampuni moja ndogo ya uchapishaji wa vitabu vya sanaa hapo, niliajiriwa kama mhariri wa vitabu na niliwekwa katika bodi ya uhariri, nikishauri na kupitia vitabu kabla havijachapishwa.

"Siku moja nikiwa ofisini kwangu alikuja Pilby kunidokeza kuwa angeweza kupata "nyumba isiyo na wasi wasi kabisa" ambayo tungeitumia kufanya mazungumzo ya siri, nyumba hiyo mmiliki wake alikuwa dada mmoja wa kingereza aliyekuwa akiitwa 'Mary'(Mary halikuwa jina halisi la dada huyo, jina lake lilikuwa Muriel Gardiner), alikuwa mtalaka wa tajiri mmoja wa kiamerika, na alikuja Vienna mwaka 1927 kama mwanafunzi wa udaktari (utabibu).

Bibi huyo alikuwa na kitita cha pesa, akimiliki msitu wa miti ya mbao na akiendesha mradi huo uliokuwa jirani na Chuo Kikuu cha Vienna.

Kujitolea kwake katika harakati za wasoshalisti kulimfanya asiweze kuishi maisha ya kifahari. Alikuwa dada jasiri na mkarimu na mara nyingi alikuwa akisisitiza kulipwa kwa wahudumu ambao Halmashauri kuu ya chama cha wasoshalisti hakikuwa kikiwajali.

Pilby alijifanya ni yeye aliyemshaiwishi Muriel ajiunge na harakati zile lakini baadaye nilikuja kufahamu kuwa dada huyo aliingizwa chama hicho na Ilse Kulczar, mmoja wa viongozi wa ndani kabisa wa harakati hizo.

Baadaye nilikuja kufahamu kuwa Pilby alikuwa Double Agent ambaye wakati akisaidia harakati za makundi ya masoshalisti alikuwa pia akijihusisha na upande wa wapinzani, makomunisti.

Itaendelea toleo lijalo
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook