MAKAO Makuu ya Umoja wa Ulinzi wa Kiislamu (FPI), yaliyoko kwenye visiwa vya Molucca, yanaonekna kama ni eneo la kupumzikia zaidi kuliko kituo cha kuongoza mapambano.
Abu Bakar Wahid, kiongozi wa FPI anaendesha shughuli zake kwenye ofisi iliyojengwa kwa mabati, ndani ya kisiwa kilicho kimya cha Tidore. Hicho ni moja ya mamia ya visiwa vinavyofanya fungamano la Molucca, ambavyo vimejichawanya eneo kubwa la bahari, mashariki ya Indonesia. Jengo hilo liko kwenye ufukwe uliojaa minazi, chini ya Volcano ya Kiematubu.
Kutoka hapo kiongozi huyo mwenye miaka 49 ana uwezo wa kuona vyema, kisiwa cha karibu cha Halmahera, masafa kutokea alipo.
Halmahera imekuwa ni kituvo cha mapambano ya umwagaji damu mbaya uliodumu kwa miezi 18 sasa. Kwa Abubakar, mapigano hayo si chochote pungufu kuliko Jihadi ya vita. Katika miezi ya karibuni amekuwa hamkani, akiwafunza vijana vita. "Napeleka watu popote pale wanapohitajika", anasema kingozi huyo wa FPI, ambaye huvaa kikowi kilichozongomezwa na vazi la kijadi lenye ukosi uliochomoza.
"Kama ambavyo wapigania uhuru wetu waliokuwa na silaha duni, walivyowashinda askari waliokuwa na silaha bora wa Kidachi na sisi tunao uwezo wa kuwapiga mahasimu wetu", anaongeza kwa karne kadhaa Wakristo wamekuwa ndio wengi katika visiwa vya Molucca. Walipigana upande wa Wadachi katika vita vya kikoloni vya karne ya 19 na 20. Katika siku hizo visiwa hivyo vilijulikana zaidi kama visiwa vya viungo kutokana na mauzo makubwa ya nje ya karafuu na bidhaa za jamii ya nazi. Lakini kuanzia miaka 30 iliyopita, michanganyiko ya kidini visiwani humo ilibadilika sana.
Serikali ya Indonesia iliwahimiza Waislamu wa visiwa vilivyofurika watu vya Sulawesi na Java wahamie huko.
Mivutano ya kikabila na kidini pole pole ilijengeka na hatimaye kuripuka mnamo Januari 1999. Mapigano makali ya Waislamu na Wakrisato yalianza Ambon, ambacho ndio kisiwa kilichojaa zaidi watu, na kutokea hapo yamesambaa mpaka Halmahera, pamoja na visiwa vyake viwili vya Ternate na Tidore. Kiasi cha watu 4,000 wameuliwa na zaidi ya 200,000 kukimbia majumba yao. Lililo baya zaidi ni kuwa vita hivyo sasa vimeanza kuenea maeneo mengine ya Indonesia, ambako Waislamu wamekuwa wakiishi bega kwa bega na Wakristo.
"Ikiwa machafuko hayatadhibitiwa", anasema Afisa mmoa wa Ubalozi wa Maghabiri nchini Indonesia "basi hapo tena unaweza kuibusu Indonesia kwaheri".
Abubakar hafikirii sana kuhusu picha ya kijiografia na kisiasa. Anachotaka pekee ni kupigana kwa ajili ya dini yake. Kiongozi huyo mwenye moyo thabiti anasema, tayari ameshatuma vijana 20,000 kwenda kupigana kaskazini ya Molucca. Vikundi vyengine vya wapiganaji wa Kiislamu kwa uchache 12 vinahusika na upelekaji watu, silaha, pesa , madawa na chakula kwa familia za Waislamu walioathirika, Vikundi hivyo ni pamoja na Laskar Jihad, Al-Fatah na Umoja wa vijana wa Kiislamu.
Kwa mtazamo wa Abubakar kujiunga na vita vya vijana ni muhimu kama ilivyo kwa sala ya Ijumaa. "Kijana yeyote mwenye uwezo wa kushika upanga, lazima ajiunge na jihadi", ananadi. Kwenye uwanja nje ya ofisi yake vijana wanaoonekana wenye ukakamavu wamefulika wakimsikiliza. Lengo la Afisa huyu ni kuyarudisha mikononi maeneo ya miji na vijiji vya Kiislamu ambavyo Wakristo wenye silaha waliwafukuza Waislamu zaidi ya 100,000. Hata hivyo, amedhamiria kuenda mbali ikibidi. "Ikiwa Wakristo watakataa kuwaachia Waislamu kurudi majumbani mwao, basi tutawafukuza nje ya visiwa moja kwa moja", anasema Abubakar.
Hilo halitokuwa rahisi. Mfano kaskazini ya Halmahera ambako Wakristo ni wengi zaidi na wenye silaha bora. Pamoja na hivyo Afisa huyu, anaamini nguvu ya kidini na uwezo wa kutumia panga wa vijana wake unaweza ukashinda vikwazo vyote.
Kivuli cha Rais wa zamani Suharto ambaye utawala wake wa miaka 32 ulifikia kikomo mwaka 1998 bado kinagubika mzozo wa Molucca. Wakosoaji wanasema Suharto katu hakujaribu kutanzua mizozo ya kidini na kikabila ambayo ilikuwa ikichemka chini ya visiwa hivyo vyenye milima kwa miaka kadhaa. Kikosi cha polisi cha "Transmigrasi" ambacho kilipeleka idadi kubwa ya Waislamu katika visiwa hivyo vilivyokuwa na watu wachache ndio walioharibu uwiano wa mwenendo wa ukuaji kimakazi.
Sehemu kubwa ya mapiganao ya karibu ni kwa haja ya kulipiza kisasi. Mwishoni mwa mwaka jana, wapiganaji wa Maliput, uliomo Halmahera. Kiasi cha Waislamu 70,000 walikimbilia Ternate ambako bado kuna ngome za Waingereza na Wareno wa kale, pia kuna mikarafuu na mipopoo mingi ya kibiashara. Waislamu waliwashambulia Wakristo 20,000 wa Ternate kwa mapanga na visu. Watu 31 walikufa, Makanisa 10 na nyumba kadhaa vikachomwa moto.
Waislamu wengi wenyeji wa Ternate walijaribu kuwahami marafiki zao wa Kikristo, lakini hawakuweza kuwazuia wapiganaji wa Kiislamu kuwafunga Wakristo kamba, halafu kuwazamisha kwa mawe baharini. Kwa siku chache tu mji wote ulikuwa umesafishika.
Visasi vimeendelea, Wakristo walifanya chao katika mji mkuu wa Halmahera wa Tobelo. Wakivalia vitambaa vyekundu vichwani, walivishambulia vijiji vya Waislamu. Mara moja kulingana na maelezo ya Waislamu, waliwaswaga Waislamu Msikitini halafu wakauripua kwa bomu, wengi walikufa.
Hassan Andimakulo ambaye alikurupushwa na wauaji wa Kikristo kutoka Tobelo, alipoteza jicho lake la kushoto, pale lilipopigwa na mshale wa moto wa Wakristo. Alishuhudia Wakristo waliokuwa na bunduki wakimkamata mwanawe wa miaka 20 na kumkata koo. Hassan na familia yake kubwa walikimblia msituni bila chakula wala maji. "Nimepoteza kila kitu changu", anasema Hassan ambaye sasa anaishi kwenye nyumba ya Wakristo iliyoharibiwa katika kisiwa cha Ternate, ambako walipelekwa na jeshi la Indosia.
Mpaka sasa serikali ya Indonesia ya Rais Abdurahman Wahid haijaweza kutuliza vurugu linaloongezeka. Moja ya sababu inayotajwa na watu wa dini zote mbili ni kuwa, washirika wa Suharto, wakiwemo vigogo wa jeshi wamekuwa wakitia chokochoko. Nini lengo lao? Uvurugikaji huo mkubwa wa amani utaiporomosha serikali ya Wahid, ambayo imapania kuchunga tuhuma za ubadhirifu kwa Suharto na washirika wake wengi wa zamani.
Jeshi la ulinzi la Indosia TNI nalo limeongeza tatizo. Vikosi vizima vizima katika Molucca vimekuwa kwenye kanda wakitoa kinga za risasi kwa Waislamu wenye bunduki wakati wakiwashambulia majirani zao Wakristo. Na polisi nao baadhi yao wamejiunga na Wakristo.
Kwa kuchelewa kabisa, serikali ya Jarkata imetangaza hali ya hatari Molucca na kuweka marufuku ya kuingia visiwani humo. Vizuizi vya jeshi la maji vimepunguza idadi ya wageni ambao wamekuwa wakienda kujiunga na vita. Mapema mwezi Julai, jeshi la maji lilizuia madau 17 ya uvuvi yaliyokuwa yakielekea Halmahera na kutaifisha bunduki kadhaa na Marisau yake. Jambo hilo limepelekea Abubakar na vikundi vingine vyenye silaha kutumia mbinu nyingine za kuibia.
Kamanda huyo anasema hilo si Uislamu na haina maana yoyote serikali kuivurugia FPI. "Wahid hawezi kutuzuia", anasema Abubakar, "Waislamu wanaagizwa na Mwenyezi Mungu, sio yeye. Kwa hivyo tutaendelea kupigana".
Jainal, mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 18 wa Hassan Andimakulo ana hisia hizo hizo. Ndio kwanza amerudi Ternate kwenye usalama baada ya kurudi kupigana Tobelo kwa mara ya tatu. Kijana huyu anayeonekana mwenye ari mno na uchungu amerudi nyumbani, kuja kuuguza mgu wake uliojeruhiwa. Mara atakapopona anasema atachukua silaha yake , kipanga kidogo kinachoitwa "parang" na kujiunga na rafiki zake 10 waende Tidore. Huko atasali kwenye Msikiti wa Abubakar, halafu atapelekwa Tobelo. "Nataka nipigane niutetee Uislamu, nilipize kisasi cha kaka yangu, na niirudishe familia yangu nyumbani, siogopi kufa".
Fikra kama hizo ndizo zinazopepea katika pande zote za vita hivi vya kidini.
Kutoka NEWS WEEK la Agosti 7, 2000.
Mwandishi:
RON MOREAU
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |