KUTIWA khofu, kushutumiwa na hata kupewa majina ya ajabu ajabu ni miongoni mwa mitihani watakayopata wale wote watakaoamua kuisimamisha dini ya Allah (s.w.).
Kauli hiyo ilitolewa na Ustadh Keengwa alipokuwa akichangia mada yake katika semina ya siku moja iliyowakusanya waalimu wa Kiislamu walioazimia kulihuisha somo la maarifa ya Uislamu ambalo mkoani Dodoma lilikosa walimu maalum.
"Hakuna upendeleo maalumu mtakaopata kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Misukosuko mtakayopata itakuwa ni ile ile iliyowapata Mtume na Maswahaba wake na ahadi za Allah hazitabadilika juu ya wale watakaosimamisha dini yake", amesema.
Ustaadh Keengwa aliwaambia waalimu hao kuwa wana jukumu la kuelimisha jamii kutokana na mafunzo waliyoyapata. Kushindwa kufanya hivyo watakuwa wamejisaliti nafsi zao mbele ya Allah (s.w.).
"Somo la Maarifa ya Uislamu ni somo lililopangwa kitaalamu kama vile Biolojia, Historia na kadhalika, hivyo ufundishaji wake hautaki kubabaisha, na kwa kuwa idadi kubwa ya walimu wanaoendesha somo hili ni wale ambao wametokea vyuoni kwa ngazi ya diploma, matumaini yatakuwa makubwa kuweza kuwabadilisha vijana wetu wakawa na mwamko mzuri wa kuufuata Uislamu", alisisitiza Ustaadh Keengwa.
Aidha, aliwahimiza walimu hao kuwa njia ya kuhuisha Uislamu ni nzito yenye madhila na inayohitaji subra ya hali ya juu.
Alisema misukosuko katika kusimamisha Uislamu
ni sawa na dau (ngalawa) katika bahari, na historia inajieleza wenyewe
kuwa hakuna popote duniani walipojizatiti kuusimamisha Uislamu kisha jamii
hiyo ikastarehe.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |