BARUA

Pole Ustadh Ilunga Kapungu

Ndugu Mhariri

NAOMBA japo nafasi kidogo niweze kutoa pole kwa Ustadh Ilunga ambaye wiki moja iliyopita amevamiwa na watu wasiojulikana na kumkata mapanga, kwa kweli ni masikitiko makubwa sana na huzuni isiyo na kifani kwa shambulio hilo ambalo ni wazi kwamba kwa kujua Ustadh Ilunga ni miongoni mwa wanaharakati wakubwa na wasio na khofu yeyote kwa viumbe wala serikali bali khofu kubwa ni kwa Allah.

Basi napenda kutoa pole yangu na masikitiko Wallah Wabilah damu yako ni ushahidi tosha pamoja na majeraha uliyoyapata mbele ya Allah na utakwendalipwa malipo makubwa zaidi. Pia napenda kutoa wito kwa wanaharakati kuwa makini sana hasa kipindi kama hiki uchaguzi umekaribia, ni kipindi kigumu sana na kipindi ambacho wale wanaoambiwa wana kidomodomo yaani wapunguze kasi ya kufikisha haki, na haki itaendelea kufika mpaka kiyama labda watumalize wote na hawawezi, sisi wa Allah, dini pia ni ya Allah na Allah atawadhalilisha tu InashaAllah.

Maulidi Haruna Nkumilwa,
S.L.P. 116,
Mpanda.


Alikopita tembo ni hatari

Ndugu Mhariri

TAFADHALI nina kuomba unitolee barua yangu katika gazeti lako ili niweze kutumia haki yangu ya msingi kutoa maoni chini ya iara ya 18(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rejea hotuba ya Mhe. Rais Mkapa aliyotoa Dodoma siku ya mkutano wa CCM: "Nanukuu "Ndugu wananchi sisi viongozi wa CCM tunafata njia walimopita tembo na tembo hao si wengine ni Mwalimu Nyerere pamoja na Karume."

Swali, Wananchi wenzangu tujiulize hakuna siku hata moja tembo akapita barabarani.Tembo hupita porini na akitokea mashambani, je tembo akitokea shambani hubakisha kitu? kama maboga atakula, nazi atakula, mtama atauvunja, mahindi hivyo hivyo kwa hiyo ndio njia wanayoitumia CCM.

Maana hiyo basi tuelewe yakuwa anapopita CCM hakuna usalama. Barabara hakuna, dawa ununue, daktari umnunue, barabara mbovu, polisi rushwa, mahakama rushwa,njaa kila mahali maana tembo washaharibu mazao.

Hiyo ndio njia aliyopita tembo.Mwananchi mwenzangu ukae ukijua akipita tembo mazao hakuna shambani, kwahiyo CCM ikipita maendeleo hakuna nchini.

Juma Mwishehe Muba,
S.L.P. 15005,
Sotele Kisiju,
PWANI.


Kisichotakiwa kusemwa

Ndugu Mhariri

SASA nimeelewa kisichotakiwa ni Waislamu kukumbushwa yale ya Buzuruga, ambapo Msikiti ulivunjwa vunjwa na Korani kuchanwa chanwa, kisha Mufti wa BAKWATA akadai iliyochanwa siyo Korani ni Yasini tu.

Kinachofichwa ni ukweli kuwa BAKWATA ilianzishwa na mkono wa Kanisa, maana Waislamu wote wakielewa hilo basi serikali ya CCM itakosa mshirika wa kuudumaza Uislamu.

Kinachokatazwa Waislamu kulijua ni ubaguzi wa kidini katika elimu, maana pindi Waislamu tukijua watainyima CCM kura Oktoba 29, 2000.

Kilichozuiliwa ni ukweli kuwa serikali eti isiyo dini hutumia mamilioni ya fedha kwa Christmass trees na mapombe na mazawadi wakati wa Sikukuu ya Kristimasi. Fedha za walalahoi walipa kodi wa Waislamu.

Mnazuiliwa Waislamu msije mkafahamu mahusiano ya Kanisa na serikali pamoja na CCM, Kanisa na Nyerere na jinsi Kanisa limekuwa msemaji mkuu wa serikali ya CCM. Msije mkahoji Tume ya majeshi ya kivita ya kanisa katoliki ni ya nini. Hakuna nusra tutakayoipata iwapo hatuta itumia vyema fursa ya kupiga kura.

Mwananchi,
Mbagala Charambe,
Dar es Salaam.
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook