Waislamu wachinjwa Maluku, maiti zatolewa mioyo, maini
Maluku, Indonesia

Mamia kwa mamia ya Waislamu wameuliwa kinyama kisiwani Maluku nchini Indonesia ikidaiwa ni waasi wanaotaka kujitenga.

Mauaji dhidi ya Waumini hao yanafanywa na watu wanaosemekana ni wakatoliki ambao wameripotiwa kumiliki silaha nyingi.

Taarifa hizo ambazo zinapatikana katika mtandao wa interneti,zinaeleza kuwa waandishi wa habari wameshuhudia miili iliyochinjwa, kupigwa alama ya msalaba vifuani, kutolewa matumbo, maini na mioyo.

Taarifa kutoka kisiwani humo zinafahamisha kuwa, misikiti inachomwa moto hali iliyosababisha makundi kwa makundi ya Waislamu kukimbia kuhama kwa kutumia maboti.

Katika tukio moja, imeripotiwa Watu waliosemekana kuwa ni Wakristo wa madhehebu ya kikatoliki waliuzingira msikiti mmoja kisiwani humo na kuwateketeza waislamu waliokuwemo kwa moto.Waliotaka kujisalimisha katika kadhia hiyo kwa kukimbia walipigwa risasi na kufa papo hapo.

Walioshuhudia matukio hayo ya kinyama wameeleza, katika maeneo mengine wauaji hao wakikatoliki wamekuwa wakiingia misikitini na kuchana Qur'an kisha kuwabaka wanawake juu ya kurasa za kitabu hicho walizozitapanya.

"Walisubiri msikiti ujae, kisha waliuzingira, Waislamu walipoona hali hiyo, walijitahidi kuonesha bendera nyeupe kama ishara ya amani na kujisalimisha lakini wauaji hao wakikatoliki hawakukubali, waliuchoma moto msikiti huo uliokuwa umejaa waumini.Waumini wote waliungua mpaka wakateketea kabisa", imeeleza taarifa kutoka kisiwani humo.

Aidha taarifa hiyo imesema wakati waumini hao wakiungua, wauaji hao walikuwa wakiwabaka wanawake nje ya msikiti huo.Zaidi ya Waislamu 750 waliuawa katika tukio hilo la kinyama.

Baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea kisiwa hicho wamesema, waliposhuhudia miili ya watu iliyoteketea, hawakuweza kuamini kama katika zama hizi za ustaarabu kungeliweza kufanyika ukatili wa kutisha kiasi hicho.

Wamesema mbali ya hao waliouawa msikitini, wameshuhudia watu waliochinjwa kama kitoweo buchani.

Walifanikiwa kupiga picha ya mtu aliyekuwa akichinjwa kwa kisu kuanzia sehemu ya nyuma ya shingo akiwa amelazwa chini na kushikiliwa barabara asigugumie kwa machungu.

Aidha wameeleza walishuhudia mwili wa Imamu uliowambwa msalabani ukiwa umekatwakatwa na kuwekewa kipande cha nyama ya nguruwe mdomoni.

Nalo jarida la Voice of Islam likiripoti unyama huo, limeshangaa kuona katika ulimwengu huu wa sasa wenye vyombo vya hali ya juu vya mawasiliano matukio ya kinyama ya Maluku hayaripotiwi.

"Ulimwengu haufahamu kitu juu ya Maluku wakati ambapo Vyombo vya habari vinadaiwa vimeufanya ulimwengu uonekane kama kijiji", limeandika jarida hilo.

Kutokana na mauaji hayo, Waislamu wametoa wito kwa Waumini wote duniani kuelekeza misaada yao ya hali na mali ikiwa ni pamoja na silaha kuwasaidi ndugu zao wa Maluku wapambane kuondoa madhila hayo.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook