C C M kuondoa kero ya soko
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Mhe. Benjamin William Mkapa amesema, CCM ikirejea madarakani itaondoa kero za soko la mazao.

Amesema, miaka mitano iliyopita ilikuwa ya kujenga misingi ya uchumi na kukusanya nguvu za wananchi.

Mhe. Mkapa ambaye alikuwa Mpanda juzi katika mikutano ya kampeni alisema, C C M katika kuwajali wananchi itawatafutia masoko ya kudumu.

Aidha, amesema, wale wanaodai kwamba CCM haijafanya kitu hawaishi Tanzania.

Amesema, CCM na serikali yake imefanya mengi ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mipya 500 na kuongeza ajira.

Rais Mkapa alikwenda Mpanda akitokea Pemba ambako alizindua kampeni kwa kumtambulisha mgombea wa CCM Zanziar Bw. Amani Karume.

Kabla ya kwenda Pemba, Mheshimiwa Mkapa alikuwa mjini Dodoma ambako akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kampeni hizo, aliwaambia wananchi wa Dodoma iwapo atarejea tena madarakani atahamisha Ikulu Dodoma ili kutoa nafasi ile ya Dar es Salaam kukarabatiwa.

Wakati huo huo, mgombea wa Urasi wa Tanzania kupitia Chama cha UDP, Bw. John Cheyo amesema, akichaguliwa atafuta karo na michango yote katika elimu ya msingi.

Ameahidi kuboresha uchumi na kuwezesha hali za wananchi kuwa bora zaidi.

Mhe. Cheyo alikuwa akizindua kampeni zake huko Mwanza juzi.

Akiwahutubia wananchi alisema, Rais Mkapa inafaa apumzishwe kwani amewatia umaskini Watanzania kwa kuwatoza kodi kubwa.

Amesema, toka Mhe. Mkapa aingie madarakani, kazi yake imekuwa kukusanya kodi na kulipa madeni ya nje bila kujali huduma muhimu za jamii.

Naye Mhe. Augustine Mrema, ameahidi kuwa akiingia Ikulu atamrejesha jijini ombaomba maarufu Mzee Matonya.

Bw. Mrema amesema, Matonya alionewa kurudishwa kwao Dodoma bila hatia. Amesema, yeye ni Mtanzania mwenye haki ya kuishi popote.

Bw. Mrema ambaye anagombea Urais kupitia Chama cha TLP amelalamika kwamba toka ateuliwe kuwa mgombea Urais hajapewa ulinzi.

Amesema, kutokupewa ulinzi, huenda ni njama za CC M, kwani Mkapa yeye keshapewa.

Mrema alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Drive Inn juzi, Jijini Dar es Salaam.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook