Nadharia ya Darwin ya Asili ya viumbe hai

Kufuta kasumba

Harun Yahaya anaendelea kuchambua upotofu wa nadharia ya mnyumbuliko (evolution) wa viumbe iliyobuniwa na mwanasayansi mkanusha Mungu wa Karne ya 19, Charles Robetr Darwin, nadharia ambayo, mbali na upotofu wake, mpaka leo hii bado inauzuzua ulimwengu. Hali hiyo ikitokana na nadharia hiyo kushikiwa bango na wanasayansi wengi wa dunia, wachapishaji wengi wakubwa, vyombo vyote vikubwa vya habari, wadhamini wa tafiti nyingi za kisayansi na dola zote kubwa za dunia. Ndugu msomaji usikose safu hii kila wiki kwa uchambuzi wa kisayansi na wa kusisimua juu ya uongo na hila za watangazaji na watetezi wa ile nadharia maarufu isemayo kuwa binaadamu wanatokana na nyani na sokwe. Endelea.

Iwapo mwanasayansi huyu atakuta matofali matatu katika barabara tambarare yakiwa yamepangwa moja juu ya jingine, hatoruhusu fikra akilini mwake kuwa matofali hayo yametokea yenyewe kwa bahati tu, tena kisha yakapandana moja juu ya jingine kwa bahati vile vile. Na ilivyo ni kuwa yeyote atakayeleta dai kama hilo ataonekana kuwa mwendawazimu.

Bali inawezekanaje basi watu walio na uwezo wa kuyachambua na kuyapambanua matukio ya kawaida katika maisha wachukue mielekeo isiyo na mantiki linapokuja suala la kutafakari juu ya kuwepo kwao wao wenyewe?

Ni jambo lisilowezekana kudai kuwa mielekeo hii inabebwa kwa minajili ya sayansi huhitaji kupewa nafasi sawa kila njia yenye uwezekano katika kulieleza jambo. Na pawapo na njia mbili, na iwapo uwezekano wa ukweli wa njia mojawapo utakuwa mdogo sana, mathalani asilimia moja, basi kanuni za kiakili na kisayansi zitahitaji kuwa na njia ile yenye uwezekano mkubwa, kwa mfano huu yenye asilimia tisini na tisa, ichukuliwe kuwa ndiyo njia sahihi.

Tukiweka akilini msingi huu wa uchambuzi wa kisayansi, kuna maoni ya aina mbili juu ya vipi viumbe hai wametokea hapa dunia. Ya kwanza nikuwa viumbe hai wameumbwa na Mwenyezi Mungu katika hali hii waliyonayo leo. Ya pili ni kuwa viumbe hai vimetokea kutokana na matukio ya bahati nasibu yasiyopangwa na yaliyotokea yenyewe. Huu wa pili ndio mtazamao wa madai ya wanasayansi wanamnyumbuliko.

Lakini tunapochunguza data za kisayansi, kwa mfano data zinazopatikana katika fani ya molecular biology, tunaona ya kuwa hata chembe ya uwezekano wa chembe hai (cell) hata moja, au walau moja tu ya milioni ya vijichembe vya protini (protein molecules) zinazopatikana katika chembe hai (cell) kuumbika bahati kwa bahati kama wanavyodai waamini mnyumbuliko. Na kama itakavyothibitishwa katika sehemu zinazofuata, ukokotozi wa mahesabu ya uwezekano (probability) unathibitisha mara nyingi tena na tena Kwa maana hiyo mtazamo wa wana mnyumbuliko juu ya namna viumbe hai vilivyotokea una uwezekano wa sifuri (zero probability).

Hii inamaanisha kuwa mtazamo ule wa kwanza una uwezekano wa asilimia mia moja (one hundred percent probability) wa kuwa kweli. Kwa maneno mengine uhai umeumbwa. Viumbe hai wote wametokea kwa kuumbwa na muumbaji aliyetukuka katika uwezo wake, busara na upeo wa elimu Ukweli huu si suala la imani pekee, bali ndilo hitimisho ambalo busara, mantiki na sayansi vinakofikishia.

Katika mazingira haya, mwanasayansi mnyumbuliko anapaswa kuondoa hoja yake na kuufuata ukweli ulio wazi na uliothibitika. Kuufanya vinginevyo ni mtu kuwa tayari kuitoa muhanga sayansi kwa ajili ya kutetea falsafa yake, itikadi yake na imani pofu (dogma) kulikokuwa mwanasayansi wa kweli.

Uwana maada mpofu

Imani juu ya falsafa inayodai kuwa maada imekuwepo daima na kuwa hakuna chochote kingine ila maada tu ni imani pofu. Nadharia ya evolusheni ndiyo inayochukuliwa kuwa "msingi wa kisayansi" wa falsafa hii ya kimaada na ndio maana nadharia hii inatetetwa kwa upofu wa hali ya juu ili tu kuisimamisha . Na sayansi inapotengwa, madai ya mnyumbuliko wa viumbe hutafutwa namna ipotoshwe ili iwekwe katika hali ya kuonekana kuunga mkono nadharia ya mnumbuliko wa viumbe ili tu kulinda uhai na falsafa ya umaada (materialism).

Mistari michache iliyoandikwa na mwanabaiolojia mmoja maarufu wa kituruki anatoa mfano mzuri unaotuwezesha kubaini upogo wa vipimo na dhamiri za watetezi wa nadharia ya evolusheni unaotokana na hamasa zao pofu. Mwanasayansi huyu anajadili uwezekano wa kutokea kibahati kwa cytochrome, ambayo ni moja ya vimeng'enyo (Enzymes) muhimu kabisa inayowezesha uhai kuwepo kama ifuatavyo:

"Uwezekano wa kuundika kwa cytochrome- C ni karibu sawa na sifuri. Yaani, iwapo uhai unahitaji mtiririko (ki-molekyula) wa namna fulani, basi inaweza kusemwa kuwa mtiririko huo, una uwezekano wa kutokea mara moja katika ulimwengu wote mzima. Vinginevyo uwezo fulani wa nguvu zilizo kuu ulio nje ya uwezo wetu wa utambuzi ndio utakuwa ulihusika katika kuundika kwake. Kukubali hili wazo la pili si jambo lililo muafaka kwa madhumuni ya sayansi. Kwa hivyo inatubidi kulitazama pendekezo la kwanza"(nukulu hii inapatikana katika kitabu Ali Demirsoy, Evolution and Inheritance, metakson Publishing Co, Ankara, 1984. uk. 61.

Mwanasayansi huyu anaamua kuchukulia kuwa ni muelekeo "wa kisayansi" zaidi kukubali uwezekano uliokaribu sawa na sifuri(zero Probability) kukubali uumbaji. Lakini kutokana na kanuni za kisayansi iwapo kuna maelezo ya namna mbili tofauti juu ya tukio moja na iwapo moja ya hayo yana uwezekano wa kutokea ulio karibu sawa na sifuri basi maelezo yale yaliyobaki yatakuwa ndiyo sahihi. Bali mwelekeo wake pofu wa kimaada(dogmatic materialism) unawakataza kukubali kuwepo kwa Muumba aliye mkuu. Katazo hili linamsukuma mwanasayansi huyu na wengine wengi waaminio katika imani pofu ya kimaada, kukubali madai ambayo hayaingii kabisa akilini.

Na watu wanao waamini na kuwategemea wanasayansi hao, nao hunasa na kuzibwa macho na zinguo hili la kimaada na huingiwa na kasumba na saikolojia tenge wasomapo vitabu na makala zao.

Huu mtazamo pofu wa kimaada ndio sababu ielezayo ni kwa nini wengi wenye majina makubwa katika jamii ya wanasayansi ni wakanushaji Mungu. Wale wote ambao hujikwamua kutokana na zinguo hili na wakaweza kuyatizama mambo kwa vichwa vilivo wazi huwa hawasiti kukubali kuwepo kwa Muumba. Mwanabayokemia(Biochemist) wa kimarekani, Dr. Michael J. Behe, mmoja wa majina makubwa(katika sayansi) anayeunga mkono nadharia ya uumbaji wenye hekima, nadharia ambayo sasa inakubalika sana, anawaelezea wanasayansi wapingao kuwepo kwa uumbaji ifuatayo:

"Kwa kipindi cha miongo minne iliyopita bayokemia ya kisasa imefuma siri za chembe hai(cell). Imechukua makumi ya maelfu ya watu kuweka sehemu kubwa ya maisha yao katika kazi ichushayo ya maabara... Matokeo ya juhudi hizi za kuichunguza chembe hai(cell) - kutafiti uhai katika mapeo ya kimolekula(molecular level) ni muito wa sauti kubwa, uliodhahiri na wenye kuchoma - "uumbaji wa hekima!" Matokeo yake yako bayana na yasiyo na utata na yenye umuhimu mkubwa kiasi cha kufanya yaweze kupewa daraja ya kuwa moja ya mafanikio makubwa katika historia ya sayansi... Lakini badala yake, kimya kikubwa kimeuzunguka muundo wa hali ya juu wa chembe hai(cell). Basi ni kwa nini jumuiya ya wanasayansi haipupii uvumbuzi wake wa kushangaza? Ni kwa nini wasomi hwa wanahofu kulitafiti suala la kuwepo kwa uumbaji? Tatizo linalowaweka njia panda ni kuwa wakati ambapo upande mmoja wa tembo huyu unakipeperushi chenye maandishi "mpangilio" wa uumbaji wenye hekima", upande wa pili lazima uandikwe Mungu.

Michael J. Behe Darwin's Black Box, Free Press, 1996 uk. 232-3.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook