TUNGEPENDA tuanze kwa kuwauliza Waislamu: Je, kimya chao wanaona Uislamu umekuwa balaa kwao? Uislamu ulikuja ili kuwakomboa au wadhalilike? Je, Uislamu umekuja na sera ya unyonge!
Bilal alikuwa mtumwa. Kama walivyo watumwa wengine alitii kila amri hata zile zilizomtoa katika utu wake. Hakuweza kukohoa mbele ya mabwanyenye wa Makka.
Hata hivyo baada ya kusilimu, Bilal wa leo hakuwa wa jana. Wale wale mabedui aliokuwa akiwaogopa hakuwaona chochote.
Alikuwa radhi kufa akipambana lakini sio kukejeliwa Uislamu wake na Qur'an yake.
Kwake Qur'an haikuwa 'toy' la bunduki au mwanaserere. Bali silaha halisi ya 'ku-shoot'.
Na katika Badr alihakikisha kuwa anammaliza Umayyah aliyemtia utumwani na kumdhalilisha kabla ya yeyote.
Je, ipo Qur'an ya Bilal na ya Waislamu wa leo?
Kama Qur'an ni moja ndio ile ile ya watu wa Badr, Uhud na Ahzab, vipi leo Waislamu wakubali kufanywa vikaragosi.
Kila anayetaka umaarufu basi anadhani hawezi kuupata mpaka awatukane Waislamu.
Imefikia mahali sasa imejengwa dhana kwamba Waislamu hawana akili kwa hiyo hata wakitukanwa hawawezi kuelewa mpaka atafutwe mmoja wao anayeonekana afadhali kidogo matusi hayo yapitie kwake.
Hivi karibuni mtangazaji wa Televisheni ya Taifa (TVT) alihoji kupitia kwa Prof. Ibrahim Lipumba, vipi watu wenye vibaraghashia na kanzu nao wanashiriki siasa.
Na Mtangazaji huyo sio mara ya kwanza kuuliza swali hilo. Alishawahi kuhoji tena wakati wa kipindi cha Kitimoto.
Gazeti moja limeuliza, kiburi hii anaipata wapi!
Ukimuacha Mwenyekiti wa jopo, watangazaji wote waliokuwa wakimhoji Prof. Lipumba walikuwa Wakristo. Alikuwemo Pascal Mayala, A. Nkya na wengine.
Yawezekana hii ikawa ndio sababu ya jeuri yenyewe. Anawapelekeeni salamu Waislamu; hata nyie!
Ndio ile ya Muislamu mwenye digrii ya kilimo anafanyakazi mpaka anastaafu hapati Ukatibu kwa vile Salum Khamis, mwingine mwenye cheti anakuwa Katibu Mkuu na kustaafu kama Katibu Mkuu wa Makatibu wakuu, kwa vile jina lake Timoth.
Hii ndio kibri yenyewe. Ndio ile Prof. Malima alimkuta Wizara ya Elimu Muislamu mwenye digrii mbili kapewa meza isiyo na kazi, Idara ya Mitalaa, huku Katibu Mkuu ni wa chini kwake kielimu na utendaji kazi!
Na si ajabu hata hao waliopo TVT wanajua wapo walioomba kazi hapo wakiwa na shahada ya Uzamili (Masters degree), lakini hata kuitwa tu kusailiwa hawakuitwa. Pengine waliponzwa na majina yao.
"Vipi mikutano yako wahudhurie wenye vibaraghashia", swali hili haulizwi Lipumba, ni nyinyi. Iweje na nyinyi leo mnathubutu kuingia katika siasa, mnathubutu kupiga kura na hata kutaka kuchaguliwa.
Vipi tena na vikofia vyenu na vijihijabu vyenu mnataka uongozi. Lakini kwa kuwadhania wajinga sana, hamwelewi anamwuliza Lipumba. Vipi unawaruhusu watu hawa?
Haya ni matusi mazito kwenu kama Waislamu sio kama Watanzania.
Mtangazaji na hao waliomtuma wanajua nyinyi ni Watanzania ndio maana wanawatoza kodi.
Kimya chenu Waislamu, maana yake mmekubali nyie hamna haki! Je, Uislamu umekuwa balaa kwenu? Je, mnataka kujuta kwanini mmekuwa Waislamu?
Kimya chenu mnakubali Uislamu ni balaa kwenu. Mnaruhusu kudhalilishwa?
Wakumbukeni mashujaa wa Badr, hawakupambana na akina Abujahal ili wakukabidhini Uislamu mje muuache ukejeliwe na kutukanwa.
Pamoja na kibri awezayo kuwa nayo mtu, lakini Mwenye haki yake ya kibri ni Allah (s.w.t).
Naye ndiye mwenye haki ya kuvumiliwa kwani yeye ndiye Alqahar.
Uislamu katu haumuandai muumini kuwaogopa watu kwa vyeo vyao wala maguvu yao. Na tangu hapo unauhesabu woga kuwa ni shirki na shirki haina msamaha mbele ya Allah. Suala ni kuheshimiana.
Kimya hiki tunahoji Waislamu mmeritadi? Hata kama wapo walioritadi mkabaki wachache kwani Makkah walikuwa wangapi! Walikuwa na nguvu gani!
Kuweni na yakini katika imani zenu na muwe na hakika kuwa mtakufa. Jibu lenu litakuwa nini mtakapoulizwa vipi mliruhusu watu wachukue kodi zenu kisha wakutukaneni!
Mnadhani hawa wangemkuta Bilal mmoja tu hapa,
wangekuwa na kibri hii na kutamba!
--
![]()
|
|