Ndugu Mhariri
NAOMBA nafasi katika gazeti lako tukufu nitoe yangu machache. Mtu unaposema mimi mimi mtu wa ukweli na uwazi na mwadilifu maana yake mkweli na sio muongo na uwazi hufichi kitu, muadilifu mwaminifu.
Je, Ukweli, uwazi, uadilifu ndiyo huu? Mauaji ya Waislamu Msikitini Mwembechai kufuatia shinikizo la Paroko Camilus Lwambano. Kuwekwa ndani wanawake wa Kiislamu na kudhalilishwa. Kuzuia mihadhara na kukamata wahadhiri na kuwafungulia kesi mahakamani.
Kukataa kuunda Tume ya kuchunguza mauaji ya Waislamu Mwembechai, kuzuia kitabu cha Mwembechai Killings bila sababu za kimsingi. Kuwalazimisha Waislamu wakubali Yesu Mungu wakisema Yesu siyo Mungu, kamata weka ndani. Kuwazuia wasijiunga na OIC. Wananchi wa Nzasa kuchomewa nyumba zao moto na kuachwa bila hadhi.
Jee huu ndiyo ukweli, uwazi na uadilifu wa serikali hii kwa wanawake?
J. Bin Mussa Tetele,
Dar es Salaam.
Ndugu Mhariri
KATIKA somo la Uraia tumeishapewa uhuru wa kuchangia katika uendeshaji wa nchi yetu, pia uhuru katika kutoa maoni.
Raia tunao uhuru wa kikatiba kubadili uongozi mzima au mfumo wa uongozi wa Taifa letu endapo utakuwa hautendi haki za kiraia tena bila kulazimishwa kutawaliwa na chama chochote au mtu fulani. Mfano wazee wetu walidai uhuru baada ya kukataa kutawaliwa na wakiloni.
Uongozi uliopo umeshindwa kuongoza vyema, malengo yote ya kudai uhuru yamepotoshwa kama vile nchi yenye kila aina ya madini unayoyajua duniani kama dhahabu, almasi, lulu, rubi na kadhalika na umaskini uliokithiri, magonjwa, maradhi, huduma za jamii kama hospitali, shule, maji, barabara mbovu, umeme na simu na duni, hakuna ajira, pesa hakuna, biashara hakuna na kadhalika.
Nchi yetu haikuwa masikini kiasi hiki na haitakiwi kuwa masikini. Sasa wakati wa kujiuliza wananchi je, hali hii iachwe iendelee? Tutakuwa masikini mpaka lini?
Juma Stambuli,
Tabora.
|
|