MWALIMU Nyerere alikuwa hadhiri na hatari ambayo ilikuwa ikinyemelea Tanzania. Lakini kwake yeye inasemekana aliliona tatizo la Waislamu kwa mtazamo mwingine. Aliona kuwa tatizo ni Rais Mwinyi kwa kushindwa kuwadhibiti Waislamu.
Katika ufunguzi wa Kanisa Katoliki katika kijiji chake cha Butiama Nyerere akiongelea kuhusu uchaguzi wa rais wa mwaka 1995, alisema kuwa Profesa Malima, Joseph Warioba na Benjamin Mkapa wote walikuwa na uwezo wa kuiongoza Tanzania.
Nyerere alisema kuwa Profesa Malima ana usomi, uzoefu na sapoti ya Watanzania kumuwezesha kuwa rais. Hiyo yeye alisema hakatai, ripoti ilimnukuu. Hata hivyo alitoa upendeleo kwa Benjamin Mkapa na Joseph Warioba. Kati ya hao wanachama wawili Nyerere alipendekeza mmoja wao achaguliwe na CCM kugombea urais.
Katika hotuba hiyo Nyerere alimshutuma Rais Mwinyi kwa udini. (Angalia: Bahari, Juni 19-25 1995). Nyerere alisema ni kazi ya kiongozi atakaekuja baada ya Rais Mwinyi kuondoa tatizo hili la udini. (Angalia: Kiongozi, Januari 1-15 1994; Vilevile Al-Bayan No. 2, 24 Mei 1994). Kwa hakika kwa udini Nyerere hakuwa anamaananisha Ukatoliki kwani huo ulikuwa umeshamiri katika serikali na Bunge la Jamuhuri kwa asilimia sabini (70%) kama alivyoeleza Padri Sivalon.
Kwa udini Nyerere alikuwa amekusudia Uislamu. Inaelekea Nyerere alikuwa anamtaka rais atakaekuja kuwashughulikia Waislamu.
Katika utawala wa Rais Mwinyi Waislamu walikuwa na fursa ya kupumua zaidi. Waislamu walijiimarisha sana katika mihadhara ya wazi.
Kutokana na ushindi huu Kadinali Otunga wa Kanisa Katoliki Kenya, alitoa onyo kuwa Ukristo utakufa endapo Kanisa halitazuia mihadhara ya Waislamu (Angalia: The Standard, (Nairobi), 13 Januari 1993).
Kufuatia kauli hii ya Kadinali Otunga, tarehe 28 Februari 1993 Tanzania Episcopal Conference (TEC) ikatoa onyo kuwa endapo mihadhara ya Waislamu haitakoma damu itamwagika. Hii ilikuwa mara ya pili kwa Kanisa kutishia kumwaga damu. Mara ya kwanza kwa Wakristo kutoa kauli hiyo ilikuwa mwaka 1989.
Kauli hii ilitolewa na CCT ikionya kuhusu mihadhara ya Waislamu. (Angalia Lengo (Nairobi), Toleo la Kwanza No. 198, Julai 1989. Vilevile angalia makala ya Warsha ya Waandishi wa Kislamu, "Kanisa na Utulivu wa Dini Tanzania?" 22 Agosti 1989).
Kauli zote hizi zilikuwa zikielekezwa kwa serikali ili itoe msaada kulisaidia Kanisa lisije likasambaratishwa na Uislamu.
Kama suala lilikuwa ni kupunguza nguvu ya Uislamu basi Nyerere hakuweza kumtegemea Profesa Malima kumsaidia katika hilo.
Nyerere aliona njia ya kulimaliza tatizo la udini wa Waislam ni kupata rais Mkatoliki kuongoza nchi katika awamu ya tatu. Nyerere kwa ajili hii akajitwisha mzigo wa kuurudisha madarakani uongozi wa Wakatoliki uliokuwa nje ya ulingo kwa miaka kumi kuongoza tena Tanzania.
Katika moja ya hisani nyingi alizofanyia kanisa lake ni kulihakikishia kuwa analipa upendeleo maalum na akatimiza ahadi yake kwa vitendo. Nyerere hakuwa ameridhika na jinsi serikali ya Mwinyi ilivyokuwa ikiendesha mambo.
Baada ya kifo cha Edward Sokoine Nyerere aliona hakuna atakaeweza kushika nafasi yake ila Salim Ahmed Salim.
Ifahamike kuwa Sokoine alikuwa Mkatoliki ingawa alielemea zaidi katika mila za Kimasai kuliko Ukatoliki. Wakati akiwa Waziri Mkuu Sokoine alipokuwa akitekeleza sera yake ya nguvu kazi, moja ya kazi ambazo aliziorodhesha hazitambuliki na serikali yake ilikuwa ualimu wa madras. Viongozi wa Kikristo kwa hakika hawana hisia za Waislamu.
Kwa wakati ule hapakuwa na njia ambayo Nyerere angeliweza kumkwepa Salim na wananchi wakamuelewa. Hata hivyo siasa za Zanzibar katika mkutano mkali wa vidole machoni Dodoma, CCM ikamtupa nje Salim kwa kuwa hakuwa mwana ASP bali alikuwa 'comrade' wa Umma Party. Vilevile wapinzani wake walidai ni 'Muarabu' ingawa si katika daraja la Sultan Jamshid bin Abdulla. Walioongoza kampeni dhidi ya Salim walikuwa wanachama wa Baraza la Mapinduzi wakiongozwa na Seif Bakari na Hassan Nassor Moyo. Lakini sababu ya maana hasa ni kuwa haikuwezekana aachwe Ali Hassan Mwinyi kwa kuwa yeye tayari alikuwa rais wa Zanzibar.
Hata hivyo Nyerere akiwa mwanasiasa hodari alifanikiwa kumpenyeza Warioba kama Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.
Warioba alikuwa anatoka kijiji kimoja na Nyerere. Uteuzi wa Warioba uliwashangaza hata baadhi ya vigogo vya CCM. Kwa kumpenyeza Warioba kuwa msaidizi wa Mwinyi halikuwa jambo la busara sana kwa Nyerere kwa kufanya hivyo alikuwa amekiuka utaratibu wa kuachiana madaraka katika CCM. Nyerere alikuwa amewakiuka wanasiasa wakongwe kama Rashid Kawawa, Cleopa Msuya, Daudi Mwakawago na wengineo wengi.
Nyerere hakuishia hapo, inasemekana alimpa Mwinyi orodha ya watu ambao alimweleza wangefaa kuwemo katika baraza lake la mawaziri.
Profesa Malima juu ya elimu yake kubwa hakuwemo katika ile orodha ya Nyerere kwa Rais Mwinyi. Inasemekana Mwinyi alipuuza baadhi ya ushauri wa Nyerere. Huku ndiko kulikosababisha Profesa Malima kuwapo katika serikali ya Rais Mwinyi. Hili lilimkera Nyerere. Kwa kipindi chote cha utawala wa Mwinyi Nyerere alimstahamilia tu na wakati mwingine alishindwa na akawa akimpiga Rais Mwinyi vijembe vya wazi kabisa. Nyerere akawa moja ya vyanzo vya propaganda mbaya dhidi ya Rais Mwinyi.
Lakini ili aweze kumpata rais Mkatoliki ilibidi awali ya yote apangue safu ya uongozi uliokuwapo katika CCM. Bila ya kufanya hivyo ingelikuwa vigumu sana kumpata rais amtakae yeye kwa sababu uongozi wa juu katika CCM haukuwa na tatizo katika suala la kuachiana madaraka.
Chama kilikuwa ni kikongwe na kilikuwa na utaratibu unaoeleweka wa kuweka viongozi madarakani. Aliyetegemewa kuchukua uongozi alikuwa John Samuel Malecela, Muanglikana.
Kisa cha kuporomoka kwa Malecela ni mashuhuri hakihitaji maelezo mengi. Nyerere alimuandama Malecela hadi Mwinyi akamuondoa madarakani kutokana na kile Nyerere alichodai ni 'uhuni' wa Malecela. Malecela ameingia katika historia ya Tanzania kuwa ndiye kiongozi wa mwanzo kuondolewa madarakani kwa 'uhuni'.
Nafasi ya Makamu wa rais ikachukuliwa na Cleopa Msuya na ile ya ukatibu wa CCM aliyokuwanayo Horace Kolimba akapewa Lawrence Gama. Nyerere alikuwa imeshamdhihirikia kuwa mwelekeo wa Waislamu umebadilika na hawaiitikadi CCM kama chama chao kama ilivyokuwa TANU.
Nyerere alikuwa hadhiri kuhusu msuguano baina ya serikali na Waislamu na hali ya hatari ambayo ilikuwa ikinyemelea Tanzania.
Mkapa hakuwa katika kundi la wana-CCM wa ndani ambao mtu angelitegemea angeweza kushika uongozi wa juu si katika CCM wala kuongoza nchi. Warioba hakuwa na uzito wowote. Yeye aliwekwa katika nafasi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.
Warioba hakuwa na uzito wowote si ndani ya CCM wala katika serikali kiasi cha kuwa katika kesi ya uchaguzi wa mwaka 1990 katika jimbo la Ikizu, alipata kushitakiwa na Mohamed Nyaobwa. Inasemekana Nyaobwa alishawishiwa kwa hongo ajitoe ili Warioba akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais apite bila kupingwa ili kutoa sura ya kuwa Warioba alikuwa akipendwa na wananchi. Nyaobwa alikataa kutoa jina lake.
Mahakama ilielezwa kuwa kulikuwa na ushawishi wa hongo na vitisho dhidi ya Nyaobwa kutoka katika uongozi wa juu wa CCM Musoma. Mwinyi alimng'oa Warioba katika serikali yake na nafasi yake akampa John Malecela. Huu ndiyo ulikuwa kigezo cha uwezo wa Warioba na umaarufu wake.
Nyerere alisema ni kazi ya kiongozi atakaekuja baada ya Rais Mwinyi kuondoa tatizo hili la udini. Kwa hakika kwa udini Nyerere hakuwa anamaananisha Ukatoliki.
Kwa udini Nyerere alikuwa amekusudia Uislamu. Kama suala lilikuwa ni Uislamu basi Nyerere hakuweza kumtegemea Profesa Malima kumsaidia katika hilo. Kwa ajili hii basi ni wazi Malima au Muislamu yeyote hata Jakaya Mrisho Kikwete asingefaa kutawala.
Katika mazingira kama haya ni historia tu ndiyo
itakayoweza kuja kuelezea ni katika mazingira gani Mkapa aliletwa madarakani
na Nyerere kuja kuchukua uongozi wa nchi.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |