Tuchague haki sawa kwa wote

Ndugu Mhariri

Naomba nafasi nitoe machache kuhusu uchaguzi wa Oktoba 29, 20000 kwa Waislamu.

Waislamu lazima tuelewe ili tusijekupata laana ya Mwenyezi Mungu. Sisi Waislamu hatupigi kura ili kumpata kiongozi atakayesimamia sheria za Kiislamu.

Bali Waislamu wote nchini tupige kura kama mkataba wa kupatiwa haki sawa kwa watu wote. Asiyetaka haki aelimishwe.

Ally R. Mpendu,
Keko - Mwanga,
Dar es Salaam.



Achaneni na CCM

Ndugu Mhariri

NAOMBA nafasi katika gazeti lako tukufu la AN-NUUR ili kutoa maoni yangu.

Ningewaomba wale Waislamu wanaolisoma gazeti hili kusoma kisa cha Bilal alivyokuwa akiteshwa na makafiri kumtaka akubali masharti ya hao makafiri. Sasa Waislamu Chama cha CCM mambo inayoyafanya ni sawa na kisa hiki, kwa sababu kinalazimisha watu kukikubali uongozi wao kwa hiyo Muislamu kukubali uongozi wa CCM itakuwa amekuunga mkono mambo haya yafuatayo:

Itakuwa umeunga mkono unyanyasaji wanaofanyiwa Waislamu hapa nchini.

Utakuwa umekubali mauaji ya Waislamu yaliyofanyika Msikiti wa Mwembechai.

Utakuwa umekubali kuwa kwa Muislamu Tanzania si lolote si chochote.

Kwa maoni yangu binafsi naiusia nafsi yangu na kuwausia Waislamu wenzangu kuyaangalia haya na dawa yake ni kutokuchagua CCM.

Mashaka Bamila,
Turiani,
Morogoro.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook